LUANDA: Ugonjwa sawa na Ebola wauwa watu Angola.
23 Machi 2005Matangazo
Shirika la afya duniani WHO limetangaza kuwa ugonjwa uliozuka nchini Angola na unaowaathiri zaidi watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ni sawa na ugonjwa wa Ebola.
Zaidi ya watu 90 wamekufa nchini Angola kutokana na ugonjwa uliofanana na Ebola na dalili zake ni pamoja na kutapika, kuhara damu na homa kali.
Watalaamu wa matibabu wamesema kuwa wamepokea wagonjwa mia moja na moja wenye dalili za ugonjwa huo katika mji wa Uige.
Shirika la afya duniani limepambana na mikurupuko ya ugonjwa wa Ebola tangu mwaka 2000 barani Afrika.
Waziri msaidizi wa afya nchini Angola Jose Van Dunem amesema kuwa serikali ya Angola imeongeza wahudumu wa afya katika mji wa Uige ili kusaidia kuikabili hali hiyo.