1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luis Enrique kocha mpya wa Uhispania

Sekione Kitojo
9 Julai 2018

Kocha wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ameteliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya Uhispania

FC Barcelona Luis Enrique
Kocha mpya wa Uhispania Luis EnriquePicha: Getty Images/D. Ramos

Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  Barcelona  Luis Enrique ametia saini mkataba  wa  miaka  miwili  kuchukua  hatamu za kuifunza  timu ya  taifa  ya  Uhispania. Anachukua  nafasi  ya  Julen lopetegui, ambaye  alifutwa  kazi katika  mkesha  wa  kuanza  kwa  fainali  za kombe  la  dunia  baada  ya  kukubali kazi katika  timu  ya  Real Madrid.

Fernando Hierro alichukua  udhibiti wa  timu  hiyo  kwa  muda  kwa ajili  ya  fainali  hizo, ambapo  mabingwa  hao  wa  mwaka  2010 wa kombe  la  dunia  waliondolewa  katika  awamu  ya  mtoano na wenyeji Urusi.

Mwandishi: Sekione Kitojo / dpae / afpe / rtre
Mhariri: Mohammed Khelef

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW