Lukaku aikoa Inter dhidi ya Gladbach ligi ya Mabingwa
22 Oktoba 2020Lukaku aliiweka Inter mbele baada ya kupachika bao kunako dakika 49 huko San Siro kwa kilabu cha Bundesliga kikitoka nyuma na kupachika bao kwa njia ya penalti kunako dakika ya 63 kupitia Ramy Bensebaini na Jonas Hofmann akipachika wavuni bao la pili dakika sita badaye.
Lakini, Lukaku alipata fursa ya kupachika bao katika dakika za lala salama. "Kwangu matokeo ya leo sio mazuri, kwa sababu tunaweza kufanya vizuri zaidi. Lazima tuendelee kufanya kazi na kuwa na nguvu ya kiakili," alisema Lukaku.
"Sio wakati rahisi kwetu, lakini lazima tuendelee kuamini ubora wetu." Lazima tuwe na nguvu na katika ulinzi tunapaswa kufanya vizuri pia. Tuliruhusu mabao mawili kwa sababu ya makosa yetu, tukapoteza nafasi nyingi. Katika michezo kama leo."
Mapema, katika Kundi B hilo hilo, Shakhtar Donetsk alikwenda kileleni baada ya kuishtua Real Madrid kwa kuichabanga mabao 3-2 huko Uhispania. Inter ni ya tatu kwenye kundi nyuma ya Borussia Moenchengladbach.
Antonio Conte alididimiza matumaini ya Inter Milan kurudi mchezoni baada ya kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa AC Milan wiki iliyopita, lakini walikuwa wakipata tabu kufuatia kukosekana kwa wachezaji wao watano kufuatia kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona.
Hakimi alitengwa saa chache kabla ya mchezo
Beki wa pembeni Achraf Hakimi alitengwa saa chache kabla ya mchezo, akiungana na wachezaji wengine wanne wa Inter baada ya kukutwa na maambukizi ya virusi vya corona Milan Skriniar, Roberto Gagliardini, Andrei Radu na Ashley Young.
Hakimi alijiunga na washindi wa tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Inter kutoka Real Madrid katika msimu wa joto na alikuwa amevutia katika mechi zake za ufunguzi. "Haikuwa rahisi leo kupokea habari saa 5:00 usiku kwamba Hakimi alikutwa na maambukizi ya virusi vya corona," alisema Conte.
"Alifanya mazoezi na sisi hadi asubuhi ya leo, tulikuwa tumejiandaa. Lakini niliwaambia vijana hawa wakabiliane na hali hii moja kwa moja. "Tulicheza vizuri dhidi ya timu ambayo ina uwezo mkubwa. "Sikumbuki uokoaji wowote wa Handanovic wakati tulikuwa na nafasi za kushinda mchezo. Sina la kukosoa vijana hawa."
Matteo Darmian alichukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Morocco Hakimi na Dane Christian Eriksen akianzia nyuma ya Lukaku na Alexis Sanchez, ambaye alipendelea kuanza juu ya Lautaro Martinez.
Alessandro Bastoni alirudi kwenye kikosi baada ya kupona kutokana na maradhi ya corona, na akitokea benchi katika kipindi cha pili.
Kocha wa Borussia Marco Rose aliwachagua Breel Embolo, Hofmann na Marcus Thuram kumuunga mkono Alassane Plea.
Inter walikuwa bora zaidi katika kipindi cha kwanza na Lukaku alipoteza nafasi kabla tu ya mapumziko, akiunganisha krosi ya Sanchez, kupeleka mpira kwenye uso wa lango.
Chanzo/AFP