1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lukashenko adokeza kupelekwa silaha za nyuklia kutoka Urusi

26 Mei 2023

Rais wa Balarus Alexander Lukashenko amedokeza kwamba silaha za nyuklia zinazotoka Urusi tayari zinapelekwa nchini humo, baada ya mataifa hayo mawili kusaini makubaliano ya kupelekwa silaha hizo.

Alexander Lukashenko
Picha: Mikhail Klimentyev/Kremlin/Sputnik/REUTERS

Udhibiti wa silaha hizo bado utabakia kwa Moscow.

"Ilikuwa ni juu ya Rais Vladimir Putin kunijulisha kuwa ametia saini amri juu ya hatua yetu ya kupeleka silaha za nyuklia Belarus. Tulikuwa tunazungumza juu ya hati maalum. Ndio, uamuzi ulichukuliwa ili kuendeleza kile kilichozungumzwa tu. Tulilazimika kuandaa maeneo ya kuhifadhi na mambo mengine huku Belarus. Tulifanya haya yote. Ndio maana vichwa vya nyuklia vilianza kuhamishwa," alisema Lukashenko.

Ukraine: Urusi inaishikilia Belarus kama mateka wa nyuklia

Rais wa Urusi Vladimir Putin mapema mwaka huu alitangaza kupelekwa kwa makombora ya masafa mafupi nchini Belarus, katika hatua inayochukuliwa kama onyo kwa mataifa ya Magharibi yanayoongeza usaidizi wa kijeshi nchini Ukraine.

Mpinzani wa Lukashenko, Sviatlana Tsikhanouskaya amelaani hatua hiyo na kuyaomba mataifa washirika kuchukua hatua za kuizuia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW