Lukashenko akutana na Kim Jong Un Korea Kaskazini
25 Machi 2026
Haya yanafanyika huku nchi hizo mbili ambazo zinakabiliwa na vikwazo vya nchi za Magharibi zikiwa na ukaribu na Urusi na masuala ya ukiukaji wa haki za binadamu.
Shirika la habari la kitaifa la Belarus limesema lengo la ziara hiyo ya siku mbili ya Lukashenko ni kuzidisha uhusiano wa nchi hizo mbili na kutambua maeneo wanayoweza kushirikiana na miradi wanayoweza kuitekeleza.
Mataifa yote mawili yameisaidia Urusi katika vita vyake nchini Ukraine huku Korea Kaskazini ikipeleka wanajeshi wa ardhini na silaha huku Belarus, ikiwa ilitumika kama eneo la Urusi kuanza uvamizi wake wa Ukraine mwaka 2022.
Korea Kaskazini imewekewa vikwazo vingi na mataifa ya Magharibi hasa kutokana na mpango wake wa nyuklia na majaribio yake ya makombora lakini pia kwa kuiunga mkono Urusi huko Ukraine.