Lukashenko asema hatawazuia wahamiaji kuingia Umoja wa Ulaya
19 Agosti 2024Matangazo
Lukashenko amesema hawezi kuwekewa vikwazo na umoja huo na wakati huo huo ategemewe kuwazuia wahamiaji wasiingie kwenye ukanda huo.
Kiongozi huyo wa Belarus ameyasema hayo leo Jumatatu alipofanya mahojiano na televisheni moja ya Urusi.
Mamlaka za Umoja wa Ulaya, hasa Poland zimekuwa zikiwatuhumu Rais wa Urusi Vladimir Putin na Lukashenko ambaye ni mshirika wake wa karibu, kwa kuwapitisha kwa makusudi wahamiaji kuingia kwenye mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya tangu mwaka 2021 na kuwapatia visa pamoja na pasi za kusafiria.