1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Lula da Silva aikosowa Ulaya kwa kutobadilika

8 Desemba 2023

Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil ameyakosoa mataifa ya Ulaya kwa kutobadilika, wakati Jumuiya ya Ushirikiano wa Umoja wa Ulaya na Amerika ya Kusini ikihitaji muda zaidi kukamilisha makubaliano ya kibiashara.

Rais Lula da Silva wa Brazil kwenye mkutano wa kilele wa Mercusor mjini Rio de Janeiro.
Rais Lula da Silva wa Brazil kwenye mkutano wa kilele wa Mercusor mjini Rio de Janeiro.Picha: Mauro Pimentel/AFP

Serikali ya Lula da Silva ilitumaini kufikiwa kwa makubaliano kwenye mkutano wa kilele baina ya Ulaya na Amerika Kusini, baada ya majadiliano ya zaidi ya miaka 20, ambayo ndani yake kunatarajiwa kuanzishwa ukanda mkubwa zaidi huru wa kibiashara ulimwenguni.

Umoja wa Ulaya unaitaka Amerika ya Kusini kuhakikishiwa ikiwa uzalishaji wa bidhaa za kilimo zitakazouzwa nje hautaharibu msitu wa mvua wa Amazon au mifumo mingine muhimu ya ikolojia.

Soma zaidi: Viongozi duniani walaani uvamizi wa majengo ya utawala Brazil

Hata hivyo, Rais Lula da Silva anasema Ulaya haitaki kubadilika na kukosoa vikali sera ya "kujilinda" ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, aliyeyapinga makubaliano hayo walipokutana pembezoni mwa mkutano wa mazingira wa COP28 huko Dubai.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW