1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

Lula kukutana na Xi mjini Beijing baada ya kuikosoa Marekani

14 Aprili 2023

Rais wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva atakutana na mwenzake wa China Xi Jinping mjini Beijing wakilenga kutanua ushirikiano baina ya madola hayo mawili

Besuch von Brasiliens Präsident Lula in China
Picha: Ricardo Stuckert/AFP

Mwanasiasa huyo wa mrengo wa shoto anaietembelea China siku chache baada ya serikali yake kuingia makubaliano na Beijing ya kufanya biashara kwa kutumia sarafu za mataifa yao badala ya dola ya Marekani.

Soma pia: Rais wa Brazil kuizuru China

Akiwa mjini Shanghai jana Alhamisi, rais Lula alikosoa kwa matamshi makali utegemezi mkubwa wa ulimwengu kwa sarafu ya Marekani na kutoa mwito kwa mataifa yanayoinukia kutafuta njia ya kufanya biashara kwa sarafu nyingine.

Mbali ya masuala ya uchumi, mkutano kati ya Lula na rais Xi utagusia pia suala la mzozo wa Ukraine katika wakati Brazil inataka tena kuchukua jukumu katika masuala ya kimataifa baada ya miaka minne ya kujitenga ilipokuwa chini ya utawala wa Jair Bolsonaro.