SiasaBrazil
Rasimu ya kwanza ya makubaliano ya Cop30 inawasilishwa
19 Novemba 2025
Matangazo
Rasimu hiyo iliwasilishwa wakati Rais Luiz Inácio Lula da Silvaalipotangaza kuwa anarudi Belem, jiji lililo ndani ya msitu wa mvua ambako mazungumzo yanaendelea, katika juhudi za kufanikisha makubaliano.Rasimu hiyo inatoa wigo wa matokeo yanayowezekana, ikionyesha tofauti kubwa kati ya takriban mataifa 200 yanayoshiriki mkutano huo katika Amazon, na safari iliyosalia kufikia makubaliano ya mwisho.Hati hiyo yenye kurasa tisa inashughulikia maeneo makuu yenye mvutano huko Belem: hatua za kibiashara, madai ya ufadhili zaidi kwa mataifa maskini, na upungufu wa ahadi za kitaifa za kupunguza hewa ya ukaa.