Lumbala atangaza mgomo wa kula kupinga kesi dhidi yake
15 Novemba 2025
Matangazo
Lumbala, ambaye aliwafukuza mawakili wake na kukataa kufika mahakamani baada ya siku ya kwanza ya kesi Jumatano akidai kuwa mahakama hiyo ya Ufaransa haina uhalali wa kumshtaki, alitangaza mgomo wake wa kula katika taarifa iliyosomwa na mkuu wa mahakama ya jinai ya Paris, Marc Sommerer.
Hata hivyo Daniele Perissi, mkuu wa mpango wa Kongo katika shirika lisilo la kiserikali TRIAL International, moja ya makundi yanayowakilisha asasi za kiraia, ameliambia shirika la habari la AP kwamba mbinu za Lumbala zinalenga kuvuruga na ni juhudi za kuepuka uwajibikaji. Ameitaka mahakama hiyo kuhakikisha kwamba haki iliyocheleweshwa haizuiwi kutekelezwa. Wizara za sheria za Kongo na Ufaransa hazijatoa tamko kuhusu hali hiyo.