1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUSAKA:Chiluba kushtakiwa kwa wizi wa fedha

8 Desemba 2003
Rais wa zamani wa Zambia Fredrick Chiluba hapo kesho atafikishwa mahkamani kwa madai kwamba ameiba mamilioni ya dola kutoka katika hazina za taifa hiyo ikimaanisha kukamilika kwa hatua ya kupiga vita rushwa inayoshinikizwa na mtangulizi wake na ambaye wakati fulani alikuwa mfuasi wake mkubwa Rais Levy Mwanawaswa. Chiluba ambaye alikuwa Rais kuanzia mwaka 1991 hadi mwaka 2001 atafikishwa mahkamani pamoja na washtakiwa wenzake sita ambao ni mkuu wa zamani wa ujasusi,balozi wa zamani kwa Marekani, wafanya biashara wawili na watumishi wa serikali wawili. Watakabiliwa na mashtaka 169 ya wizi, rushwa na kutumia vibaya madaraka yenye kuhusisha zaidi ya dola milioni 29.Mojawapo ya mashtaka hayo ni kwa shirika la ujasusi la Zambia kuweka fedha kwenye akaunti za benki nchini Uingereza zilizochukuliwa kutoka wizara ya fedha. Wapelelezi walifunga madarzeni ya akaunti za aina hiyo na kutaifisha mali.
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW