1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Luxembourg kunafanyika uchaguzi wa bunge

8 Oktoba 2023

Leo hii kumefanyika uchaguzi wa wabunge huko Luxembourg, taifa dogo, tajiri la Umoja wa Ulaya lenye wapiga kura 284,000 tu.

Serbien | Der luxemburgische Premierminister Xavier Bettel
Picha: Amir Hamzagic/AA/picture alliance

Tangu mwaka 2013 taifa hilo linatawaliwa na muungano wa vyama vitatu unaoongozwa na Waziri Mkuu wa kiliberali, Xavier Bettel.Kwa zingatio la kura ya maoni ya hivi karibuni, muungano wake na wenye kuhusisha vyama vya Greens and Social Democrats ambao kwa sasa unashikilia viti 31 kati ya 60 bungeni, unaweza kupata kura za kutosha kudumisha wingi wake kwa muhula mwingine madarakani.Hata hivyo, chama cha upinzani cha Christian Social People's Party, ambacho kimeingia kwenye kinyang'anyiro hicho na  mgombea wake mkuu Luc Frieden kimetajwa kuongoza katika kura za maoni.Kupiga kura ni lazima katika taifa hilo la pili kwa udogo katika Umoja wa Ulaya likiwa na jumla ya watu 660,000 huku wengine 88,000 wanaoishi nje ya taifa hilo wakiwa na msamaha wa kutoshiriki zoezi hilo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW