Luxembourg. Mawaziri wataka wakimbizi wa Iraq wasaidiwe zaidi.
20 Aprili 2007Matangazo
Mawaziri wa mambo ya ndani wa umoja wa Ulaya wanakutana mjini Lexembourg leo Ijumaa kwa kujadili njia mpya za kuwasaidia wakimbizi kutoka Iraq.
Umoja wa Ulaya uko katika mbinyo kutoka kwa mashirika ya kutoa misaada kuchukua wakimbizi zaidi kutoka Iraq hatua ambayo itapunguza mzigo kwa nchi jirani kama Syria na Jordan, ambazo zina wakimbizi zaidi ya milioni mbili baina yao.
Sweden inatarajiwa kuutumia mkutano huo wa umoja wa Ulaya kuhimiza umoja zaidi katika kuwahifadhi wakimbizi kutoka Iraq.
Kiasi cha wakimbizi 20,000 kutoka Iraq wameomba hifadhi katika mataifa ya umoja huo katika mwaka 2006 ikilinginishwa na mwaka 2005 , ikiwa ni ongezeko la asilimia 77.