1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBOURG: Mkutano kuhusu Iraq kufanywa mwezi Juni

17 Aprili 2005

Umoja wa Ulaya utatayarisha mkutano wa kulijadili suala la Iraq,mjini Brussels mnamo mwezi wa Juni.Tangazo hilo lilitolewa na waziri wa mambo ya kigeni wa Luxembourg,Jean Asselborn baada ya kuwa na mazungumzo ya siku mbili pamoja na mawaziri wa kigeni wa Umoja wa Ulaya.Luxembourg hivi sasa imeshika wadhifa wa rais wa Umoja wa Ulaya unaozungushwa.Mjumbe wa Umoja wa Ulaya kuhusu masuala ya kigeni,Benita Ferrero-Waldner amesema mkutano wa aina hiyo ni "muhimu" kwa mustakabali wa Iraq iliyoathirika kwa vita.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW