LUXEMBOURG : Solana kukutana na Larijani
24 Aprili 2007Matangazo
Mratibu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya Javier Solana ameelezea matumaini yenye tahadhari juu ya mkutano wake wa hapo kesho mjini Ankara Uturuki na msuluhishi wa masuala ya nuklea wa Iran Ali Larijani.
Hili ni jaribio jiipya kabisa la Umoja wa Ulaya kuishawishi Iran kusitisha shughuli zake za kurutubisha uranium.Na pia ni jaribio la mwanzo tokea Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuidhinisha duru ya pili ya vikwazo dhidi ya Iran kutokana na mpango wake wa nuklea.
Solana alikuwa akizungumza pembezoni mwa mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya mjini Luxembourg muda mfupi baada ya kuidhinisha vikwazo vipya vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran.