LUXEMBOURG : Ulaya yakubali sheria dhidi ya ubaguzi
20 Aprili 2007Matangazo
Mawaziri wa sheria wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Luxembourg wamekubaliana juu ya sheria ya pamoja dhidi ya ubaguzi ambayo hata hivyo imepungzwa makali.
Maafisa wa Umoja wa Ulaya wamesema kufikiwa kwa muafaka huo kunaonyesha tafauti kubwa miongoni mwa nchi wanachama 27 wa umoja huo juu ya namna ya kupambana na ubaguzi na uhalifu unaosababishwa na chuki.
Mojawapo ya hatua zilizokubaliwa kuchukuliwa na mawaziri hao wa sheria ni kifungo gerezani dhidi ya wale wanaokanusha au kupuuza Maangamizi ya Wyahudi.
Uchochezi wa chuki au matumizi ya nguvu dhidi ya watu kutokana na makabila yao, dini au utaifa wao utaadhibiwa kwa kifungo cha hadi miaka mitatu gerezani.
Hata hivyo itakuwa ni kwa mataifa wanachama kujiamulia kuwachukulia hatua wale wakosaji wakubwa tu.