LUXEMBURG-Umoja wa Ulaya waonesha wasiwasi juu ya haki kutendeka katika uchaguzi wa Bunge wa Zimbabwe.
30 Machi 2005Ikiwa imesalia siku moja kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Wabunge nchini Zimbabwe,Umoja wa Ulaya,umeonesha wasiwasi wake juu ya haki kutendeka katika uchaguzi huo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Lexemburg,Nicolas Schmit ameliambia Bunge la Ulaya,kuwa uchaguzi huo unaonekana hautakidhi viwango vinavyotakiwa na jumuia ya kimataifa.Luxemburg kwa hivi sasa ndio inakalia kiti cha urais wa Umoja wa Ulaya.Bwana Schmit pia amesema Umoja wa Ulaya utaichukulia hatua serikali ya Harare haraka iwezekanavyo,ingawa hakufafanua zaidi juu ya hatua hizo.
Rais Rober Mugabe wa Zimbabwe amekwishaeleza tangu awali haofii iwapo chama chake cha ZANU-PF kikishindwa katika uchaguzi huo.Rais Mugabe anajaribu kuionesha dunia kuwa amejirekebisha katika kusimamia utawala wa demokrasia,tangu kulipotekea vitendo vya umwagikaji damu na lawama za kuvurugwa uchaguzi mwaka 2000 na wa mwaka 2003.