1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

LUXEMBURG:Umoja wa Ulaya wapewa haki ya kuzuia mali za vikundi vya kigaidi.

21 Septemba 2005

Umoja wa Ulaya umepewa haki ya kimsingi kuzuia mali zote za watu na vikundi vinavyoshukiwa kuhusika na vitendo vya kigaidi.

Mahakama ya Umoja huo imesema uamuzi wa kuzuia mali kunaendana na azimio lililopitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na kamwe uamuzi huo hauendi kinyume na mpango wa Umoja wa Ulaya wa kulinda haki za binadamu.

Watuhumiwa wawili wa mtandao wa ugaidi wa al-Qaeda,wamepeleka malalamiko yao katika mahakama ya Umoja huo iliyopo Luxemburg na kudai kuwa Umoja wa Ulaya hauna haki ya kuzuia mali zao zikiwemo fedha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW