M23 wachukua udhibiti wa maeneo ya uchimbaji madini Kongo
19 Januari 2025Wakaazi wameliambia shirika la habari la AFP kwa njia ya simu kwamba kundi hilo lenye silaha lilichukua udhibiti wa Lumbishi, eneo lenye utajiri wa madini katika mkoa wa Kivu Kusini jana Jumamosi, kabla ya kuelekea Numbi na Shanje, maeneo mengine mawili katika jimbo jirani la Kalehe.
Soma pia: Tshisekedi akataa mazungumzo ya moja kwa moja na M23
Tangu 2021 kundi la M23 limekuwa likishikilia maeneo mengi ya mashariki yenye utajiri wa madini ya Jamuhuri ya Kidemkrasia ya Kongo.
Kulingana na shirika la kuhudumia Wakimbizi,la Umoja wa Mataifa, UNHCR, Takriban watu 237,000 wameyakimbia makazi yao tangu mwanzoni mwa Januari kutokana na mapigano kati ya jeshi la Kongo na M23.
Makumi ya watu wajeruhiwa na wengine wayakimbia mapigano mashariki mwa DRC