1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

M23 wakiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Kongo

Sylvia Mwehozi
15 Novemba 2023

Kundi la waasi la M23 limekiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waasi hao walijiondoa katika kijiji hicho mwanzoni mwa mwezi Aprili.

Kongo I M23
Waasi wa M23Picha: Guerchom Ndebo/AFP

Kundi la waasi la M23 limekiteka tena kijiji cha Kishishe mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Waasi hao walijiondoa katika kijiji hicho mwanzoni mwa mwezi Aprili, sambamba na maeneo mengine katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Duru zinasema Kijiji hicho kimekimbiwa kwa kiasi kikubwa na wakaazi wake, lakini mapigano yameendelea kwa siku mbili, kabla ya jeshi kuingilia kati.

Soma kuhusu: Jeshi la Congo lawazuia waasi wa M23 kuingia Goma

Mwakilishi mmoja wa asasi ya kiraia katika eneo hilo amethibitisha taarifa za M23 kukidhibiti Kijiji cha Kishishe tangu Jumatatu, taarifa zilizothibitishwa na vyanzo vingine viwili vya usalama.

Umoja wa Mataifa ulisema katika ripoti yake kwamba waasi wa M23 waliwaua watu 171 katika kijiji cha Kishishe Novemba mwaka uliopita, shutuma ambazo M23 imezikanusha.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW