M23 wataka waliotoroka Uvira kurejea nyumbani
12 Desemba 2025
Matangazo
Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka, ametoa wito kwa wakaazi hao kurejea nyumbani bila hofu yoyote.
Waasi hao wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda, wamethibitisha kuuteka kikamilifu mji huo wa kimkakati wa Uvira, Mashariki mwa Kongo, baada ya mapambano makali kati ya vikosi vyake na wanajeshi wa serikali.
Mapambano hayo mapya yalianza tangu mwanzoni mwa mwezi huu huku Marekani ikijaribu kutuliza hali katika mgogoro huo.
Uvira ni mji muhimu wa kibandari Kaskazini mwa mto Tanganyika na uko karibu sana na mji wa kiuchumi wa Bujumbura nchini Burundi.