1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 wauteka mji wa Kalembe mashariki ya Kongo

24 Oktoba 2024

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda waliuteka mji unaozozaniwa wa Kalembe, mashariki mwa Kongo, katika kile kilichotajwa kuwa hatua mpya ya ukiukaji wa makubaliano ya kusitisha vita yaliyosainiwa mwezi Agosti

DR Kongo | Wanajeshi katika eneo la Kirumba
Wanajeshi wa Kongo wanakabiliana na waasi wa M23 katika mkoa wa Kivu KaskaziniPicha: Alexis Huguet/AFP/Getty Images

Waasi hao waliingia tena katika mji huo wa Kalembe baada ya mapigano makali na kundi la muungano wa wapiganaji wanaoungwa mkono na jeshi la Kongo, lijiitalo Wazalendo. Duru za Usalama zimesema M23 wamekuwa wakiwasukuma nyuma wapiganaji hao kwa kutumia silaha zao zote.

Hata hivyo, msemaji wa kundi la Wazalendo, Marcellin Shenkuku, aliliambia shirika la habari la AFP jana kwamba pamoja na waasi hao kutwaa udhibiti wa moja ya maeneo yao, bado ni vigumu kusema ni nani anaudhibiti mji wa Kalembe kwa sasa.

Mashahidi wanasema wanamgambo wengine kundi hilo walijikita katika kijiji kidogo cha Ihula wakizidi kuusogelea mji mwingine wa Pinga wilayani Walikale ambako hali ya wasiwasi imezidi kuongezeka na raia wakikimbia kuelekea mji mkuu wa wilaya hiyo.