1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 yadai iiliushambulia uwanja wa ndege wa Kisangani

5 Februari 2026

Kundi la waasi wa M23 limedai kuhusika na shambulizi la ndege zisizo na rubani lililolenga uwanja wa ndege muhimu mjini Kisangani kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Waasi wa M23 wamedai kuhusika na shambulizi la droni katika mji wa Kisangani.
Waasi wa M23 wamedai kuhusika na shambulizi la droni katika mji wa Kisangani.Picha: Daniel Buuma/Getty Images

Kundi la waasi wa M23 limedai kuhusika na shambulizi la ndege zisizo na rubani lililolenga uwanja wa ndege muhimu katika jiji la Kisangani kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, kilomita mia kadhaa kutoka eneo la kawaida la operesheni za kundi hilo lenye silaha.

Serikali ya mkoa wa Tshopo, ambayo Kisangani ndio jiji kuu, ilisema Jumatatu kwamba ndege nane zisizo na rubani za adui ziliharibiwa kabla ya kufikia shabaha yao.

Shambulizi hilo liliashiria kuongezeka kwa mzozo mashariki mwa Kongo, kulingana na waangalizi, huku M23 ikiwa haijafanya mashambulizi hapo awali mbali na eneo lililo chini ya udhibiti wake.

Madai yalitolewa jana na  kundi hilo linaloipinga serikali ya mjini Kinshasa na linaloungwa mkono na Rwanda lilikuja siku moja baada ya tangazo kwamba Umoja wa Mataifa utatuma ujumbe katika eneo hilo tete hivi karibuni kusaidia kutekeleza usitishaji mapigano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW