1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

M23 yawalazimisha raia wa DRC kujiunga na kundi hilo

10 Juni 2026

Shirika la Human Rights Watch lasema waasi wa M23 waendesha mkakati wa kuwasajili kwa nguvu kwenye kundi hilo raia,wanajeshi na hata wapiganaji,na kuwazuia chini ya mazingira ya kikatili

Kundi la waasi la M23 limekuwa likishikilia eneo kubwa la Mashariki mwa DRC
Kundi la waasi la M23 limekuwa likishikilia eneo kubwa la Mashariki mwa DRCPicha: Moses Sawasawa/AP Photo/picture alliance

Ripoti ya shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch, imesema kundi la waasi la  M23 linaloungwa mkono na Rwanda, limewalazimisha maelfu ya watu kujiunga na kundi hilo mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo, na kuwashikilia katika mazingira yasiyokuwa ya kibinadamu.

Ripoti hiyo iliyochapishwa leo Jumatano imebainisha kwamba maelfu ya wanajeshi wa Kongo, wanachama wa makundi ya wanamgambo na raia wamekuwa wakizuiliwa na kundi hilo.Rwanda yaikosoa Human Rights Watch kuhusu ongezeko la makaburi

Baadhi ya wanaoshikiliwa ni pamoja na watoto  wa chini ya umri wa miaka 12 ambao wamepelekwa kwenye vituo au makambi ya mafunzi ya kijeshi ambako wamekuwa wakishikiliwa chini ya mazingira mabaya kwa wiki au miezi kadhaa wakipitia ukatili wa kupigwa na hata mauaji.

Ripoti hiyo ya Human Rights Watch imetokana na mahojiano yaliyofanyiwa wafungwa 102 wa zamani waliokuwa chini ya kundi hilo la M23.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW