1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maaandamano ya usafi wa mazingira Magazetini

Oumilkheir Hamidou
7 Oktoba 2019

Maandamano kudai hatua za kupambana na mabadiliko ya tabianchi, mchakato wa kumpokonya madaraka rais Donald Trump na juhudi za kupunguza mikururo ya wakimbizi wanaoingia Ulaya ni miongoni mwa mada magazetini.

Deutschland Extinction Rebellion Aktivisten in Berlin
Picha: picture-alliance/AP Photo/M. Sohn

 

Tunaanza na maandamano ya kudai hatua zichukuliwe kukabiliana na mabailiko ya tabianchi. Shaka shaka zinasikika kama maandamano hayo si kisingizio kinachotumiwa kuficha shabaha za makundi yanayofuata nadharia fulani. Gazeti la "Allgemeine Zeitung" linaandika: "Wapigania shupavu wa usafi wa mazingira, hata kama harakati zao zinalenga kuwahimiza raia wasitii amri za serikali na kusisitiza kila wakati maandamano yao ni ya amani, hata hivyo wanashindwa kutambua hatari inayoweza kujitokeza maandamano hayo yanapotumiwa na makundi ya siasa kali za mrengo wa kushoto ambayo matumizi ya nguvu kwao ni jambo geni.

Na hivyo ndivyo ufa unavyozidi kuwa mpana katika jamii: kama inavyoshuhudiwa katika suala la wakimbizi, katika kadhia ya mabadiliko ya tabianchi pia zimeibuka pande mbili zinazotofautiana na kuhasimiana. Katika hali kama hiyo serikali kuu ya muungano inaonekana kana kwamba haina nguvu , mtu anaweza kufika hadi ya kusema kwa sehemu fulani inageuka mfungwa wa sera yake wenyewe ya  mazingira."

Gazeti la Nord Kurier linakwenda mbali zaidi na kutuhumu:"KIlicho nyuma ya neno"Extension Rebellion" au "Uasi dhidi ya maangamizi" ni nadharia na vuguvugu la umati wa watu linaloshawishiwa na kundi dogo la watu ambalo viongozi hawajulikani. Hawatishiki kama maisha ya binaadamu yataangamia. Maandamano kama hayo hayana mafungamano hata kidogo na maandamano ya kisiasa, ni maandamano yaliyoandaliwa kwa werevu mkubwa na ambayo yanaficha lengo lake. Na kilio cha jamii kiko wapi-hakuna kwasababu wanaamini ni maandamano kwaajili ya usafi wa mazingiraa na ili kulifikia lengo hilo, hatua zote zinakaribishwa."

Wademocrat wanatekeleza jukumu lao la kidemokrasi

Kitanzi kinazidi kumbana rais wa Marekani Donald Trump kwa madai ya kutumia vibaya madaraka yake. Gazeti la "Passauer Neue Presse" linaaandika: "Nafasi ya kufanikiwa utaratibu wa kumpokonya Donald Trump madaraka yake ni ndogo mno. Hata hivyo kwa kufanya hivyo wademokrat wanatekeleza hatua muhimu. Wanaudhihirishia ulimwengu kile kinachotokea, pale kiongozi wa kisiasa anapoyatumia madaraka yake kwa masilahi yake. Wanabainisha demokrasia bado inafanya kazi na wamepania kuitumia hadi mwisho."

Umoja wa ulaya na mgogoro wa wahamiaji

Ripoti yetu ya mwisho magazetini inatupeleka kaatika bahari ya Mediterenia kuuangalia mzozo wa wakimbizi. Gazeti la "Neue Osnabrücker Zeitung" linaandika: "Shinikizo la wakimbizi linazidi kuwa kubwa. Umoja wa ulaya umejiandaa kukabiliana na shinikizo hilo. La. Yadhihirika kana kwamba watu hawajajifunza kutokana na makosa ya mwaka 2015. Licha ya mikutano kadhaa ya kilele na ahadi za kila aina zilizotolewa, hakuna mengi yaliyotekelezwa. Mfumo wa pamoja wa kinga ya ukimbizi, uhamiaji na  utaratibu wa kugawana wakimbizi mpaka leo hauna dalili ya kuundwa. Na mpaka wa Umoja wa ulaya hauna kinga kuwazuwia wahamiaji kinyume na sheria. Pindi mkasa kama ule wa 2015 ukitokea tena, Ujerumani itajikuta katika hali ya upweke kuliko namna ilivyokuwa miaka minne iliyopita."

 

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/Inlandspresse

Mhariri:Yusuf Saumu

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW