1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Viongozi wa dunia waadhimisha miaka 80 ya D-Day

Angela Mdungu
6 Juni 2024

Viongozi wa mataifa ya magharibi wamekutana Alhamisi huko Normandy nchini Ufaransa kuadhimisha miaka 80 tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa Wanazi wa Ujerumani.

Kumbukumbu ya D-Day
Maadhimisho ya miaka 80 tangu kuanza kwa operesheni ya kijeshi iliyoikomboa Ulaya kutoka mikononi mwa WanaziPicha: Elizabeth Frantz/REUTERS

Kumbukumbu hiyo  maarufu kama D-Day imehudhuriwa pia na maveterani wa vita na baadhi ya viongozi wa juu wa mataifa yaliyoshiriki vita hivyo akiwemo Mfalme Charles wa Uingereza aliyeongoza maadhimisho katika eneo la makaburi la New British Normandy kwa kuweka shada la maua.

Rais wa Marekani Joe Biden, kwa upande wake ameadhimisha siku hiyo kwa kukutana na maveterani wa Kimarekani wa Vita hivyo. Alitumia nafasi hiyo kuonya kuwa demokrasia duniani kote iko hatarini na kuongeza kuwa hawatoacha kusaidia kuilinda Ukraine na kuruhusu Urusi izidi kuitishia Ulaya.

Soma zaidi: Viongozi wa Magharibi wakumbuka D-Day chini ya kivuli cha Ukraine

Naye Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron wakati wa maadhimisho hayo alimtunuku nishani ya heshima veterani wa Uingereza Chiristian Lamb aliyehusika kuchora ramani zilizofanikisha majeshi ya ukombozi kuwasili katika operesheni iliyosaidia kuiweka huru Ulaya.

Rais wa Marekani Joe Biden katika maadhimisho ya miaka 80 ya D-DayPicha: IMAGO/Bestimage

Maadhimisho hayo yaliyofanyika katika fukwe kadhaa za Normandy yalihudhuriwa pia na Mwana wa Mfalme wa Uingereza, William, iliyesifu ujasiri uliooneshwa pia na wanajeshi wa Canada  alipohudhuria kumbukumbu katika ufukwe wa Juno. Waziri Mkuu wa Canada William Trudeau, na wa Ufaransa, Gabriel Attal  na Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak.

Zelensky ashiriki kumbukumbu ya D-Day

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky alifika  pia katika kumbukumbu hiyo na amesema  atahudhuria pia mikutano muhimu inayokusudia kuimarisha taifa lake wakati huu likiwa vitani. 

Soma zaidi: Maoni: Mafunzo kutoka vita kuu ya II ya dunia

Juni 6 mwaka 1944, wanajeshi 170,000 wa nchi washirika walivuka bahari na kutua kwenye fukwe za Normandy, Ufaransa, na ikawa mwisho wa utawala wa Wanazi waliokuwa wameyakalia maeneo makubwa ya Ulaya katika Vita Vikuu vya Pili. 

Veterani wa D-Day John Roberts Picha: Gareth Fuller/PA Wire/empics/picture alliance

Mashambulizi yaliyoanza siku ya D-Day dhidi ya wanajeshi wa Ujerumani waliokuwa wakiikalia kimabavu Ufaransa, ndio operesheni kubwa zaidi ya kutokea baharini katika historia ya dunia. Operesheni hiyo iligeuza mkondo wa vita ulioendelea hadi kuangushwa kwa Adolf Hitler na utawala wake wa kinazi.

     

 

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW