Maafikiano kuhusu Mpango wa kufufua Uchumi Marekani
7 Februari 2009Matangazo
Mpango huo wa muafaka ulio na thamani ya dola bilioni 780 ulikubaliwa baada ya kufanywa majadiliano magumu kati ya pande hizo mbili.Wajumbe wa Seneti walikubali kuupunguza mpango wa awali kwa kiasi cha dola bilioni 150.
Rais wa Marekani Barack Obama amewahimiza wabunge kutochelewa zaidi kuidhinisha mpango huo wa maafikiano.Ameonya, kuwa uchumi wa nchi utakumbwa na maafa ikiwa hautopitishwa haraka bungeni. Hapo awali tarakimu zilizotangazwa zilionyesha kuwa kiasi ya watu 600,000 walipoteza kazi katika mwezi wa Januari.Sasa ukosefu wa ajira umefikia asilimia 7.6 hicho kikiwa kiwango cha juu kabisa tangu mwaka 1992.