Maafikiano ya kumaliza vita mashariki mwa Kongo
8 Februari 2013Makubaliano hayo yanalenga kumaliza umwagikaji damu unaotokana na vurugu za kikabila ambazo zimekuwa zikishuhudiwa katika eneo hilo katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita na ambazo kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, zimesababisha vifo vya watu 264 na maelfu kuachwa bila makaazi. Makubaliano hayo yamefikiwa kati ya Kanali Janvier Buingo Karairi kutoka kundi la kihutu la APCLS na Kanali Bwira mkuu wa kundi linalojiita walinzi wa Kongo, Nyunga Munyamariba mkuu wa polisi wa Lushebere kutoka jamii ya wahutu pamoja na Kanali Kapopi kiongozi wa kundi la Mai Mai Nyatura. Je makubaliano hayo yamepokelewa vipi na Jumuiya za Kiraia huko Mashariki mwa Kongo? Saumu Mwasimba amezungumza na mratibu wa Jumuiya hizo Mustapha Mwiti na alikuwa na haya ya kueleza.
Insert Interview
Mwandishi:Saumu Mwasimba
Mhariri: Josephat Charo