Maafisa 15 wa Iran wawekewa vikwazo na EU
29 Januari 2026
Matangazo
Umoja wa Ulaya umemuwekea vikwazo waziri wa mambo ya ndani wa Iran, Eskandar Momeni pamoja na mwendesha mashtaka mkuu Mohammad Movahedi Azad miongoni mwa maafisa wengine wa ngazi za juu wa Tehran.
Iran yasema Israel itawajibishwa kwa kuishambulia
Baraza la Umoja wa Ulaya limetangaza uamuzi huo hivi leo likisema maafisa 15 wakiwemo makamanda wa jeshi la ulinzi wa mapinduzi, waliowekewa vikwazo wamehusika na ukandamizaji wa maandamano ya amani na kuendesha matukio ya kamatakamata dhidi ya wanaharakati wa kisiasa nchini humo.
Umoja wa Ulaya pia unajiandaa kuliorodhesha jeshi hilo la ulinzi wa mapinduzi la Iran kuwa kundi la kigaidi.