1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Maafisa wa usalama wauawa katika ghasia za nchini Pakistan

Sylvia Mwehozi
26 Novemba 2024

Waandamanaji nchini Pakistan wanaoshinikiza kuachiliwa kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan wamewaua maafisa wanne wa vikosi vya usalama vya taifa hilo.

Pakistan | Ghasia Islamabad
Polisi wakiwarushia gesi ya machozi waandamanajiPicha: Aamir Qureshi/AFP

Waandamanaji nchini Pakistan wanaoshinikiza kuachiliwa kwa waziri mkuu wa zamani Imran Khan wamewaua maafisa wanne wa vikosi vya usalama vya taifa hilo, huku umati wa waandamanaji ukikaidi amri ya polisi na kufunga njia ya katikati mwa mji mkuu.Makubaliano ya kusitisha yafikiwa Pakistan baada ya watu 82 kuuliwa

Waziri wa mambo ya ndani Mohsin Naqvi alisema "wahalifu" waliohusika katika maandamano hayo wamewaua wanachama wanne wa kikosi cha askari wa jeshi la Rangers kwenye barabara kuu ya jiji inayoelekea majengo ya serikali.

Naye Waziri Mkuu wa Pakistan Shehbaz Sharif alisema maafisa hao "waligongwa na gari", akiongeza kuwa hayo hayakuwa maandamano ya amani bali ni "itikadi kali."

Kulingana na waandishi wa habari wa AFP, zaidi ya waandamanaji elfu kumiwaliokuwa wamejihami kwa fimbo na kombeo waliwashambulia polisi katikati mwa Islamabad Jumanne mchana, kilomita kama tatu kutoka eneo la serikali wanalolenga kulidhibiti.

Khan alizuiwa kugombea katika uchaguzi wa Februari ambao ulikumbwa na madai ya wizi wa kura, akiwekwa kando na kuandamwa na kesi nyingi za kisheria ambazo anadai ziliibuliwa ili kumzuia kurejea mamlakani.

Wafuasi wa Imran Khan wakiandamanaPicha: Anjum Naveed/AP/picture alliance

Wanajeshi wanane wameuwawa na wanamgambo wa itikadi kali PakistanLakini chama chake cha Pakistan Tehreek-e-Insaf (PTI) kimekaidi ukandamizaji wa serikali na kufanya mikutano ya mara kwa mara. Maandamano ya Jumanne ndiyo makubwa zaidi kufanyika katika mji mkuu tangu Khan alipofungwa jela mnamo Agosti 2023.

Serikali ilisema Jumatatu kwamba afisa mmoja wa polisi pia aliuawa na wengine tisa walijeruhiwa vibaya na waandamanaji mjini Islamabad siku ya Jumapili.

Mji huo mkuu umefungwa tangu mwishoni mwa Jumamosi, huku mtandao wa simu za mkononi ukikatika mara kwa mara na zaidi ya polisi 20,000 wakifurika mitaani, wengi wakiwa na ngao za kutuliza ghasia na marungu.

Serikali imewashutumu waandamanaji kwa kujaribu kuvuruga ziara ya serikali ya Rais wa Belarus Alexander Lukashenko, ambaye aliwasili kwa ziara ya siku tatu Jumatatu.  Wiki iliyopita, utawala wa jiji la Islamabad ulitangaza kupiga marufuku kwa miezi miwili mikusanyiko ya watu.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW