1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa polisi wazima maandamano nchini China

Saleh Mwanamilongo
29 Novemba 2022

Mamlaka ya China imeanza uchunguzi kwa baadhi ya watu walioshiriki kwenye maandamano ya kupinga vizuizi vya Covid-19, huku polisi wakisalia mitaani kwa idadi kubwa jijini Beijing.

China | Coronavirus - Protest in Peking gegen die Null-Covid-Politik
Picha: Koki Kataoka/Yomiuri Shimbun/AP Photo/picture alliance

Shirika la habari la reuters limeripoti kuwa mwandamaji mmoja alipigiwa simu ilikujielezea kwenye kituo cha polisi hii leo jumanne kuhusu shughuli zake za Jumapili usiku.

Kisa kingine ni cha mwanafunzi mmoja aliwasiliana na chuo chao na kuulizwa kama walikuwa katika eneo ambapo maandamano yalifanyika na kutakiwa kutoa maelezo kwa maandishi. Makazi mwingine wa jiji la Beijing amesema wametakiwa kufuta jumbe zote kwenye simu zao kuhusiana na maandamano ya mwishoni mwa wiki. Amesema Polisi ni wengi mitaani, na  polisi wamechunzuga vitambulisho vya baadhi ya watu. Mkaazi huyo ameshuhudia kukamatwa kwa moja ya marafiki zake,ambae aliachiliwa baadae.

''Haki na uhuru lazima vitumike ndani ya mfumo wa sheria''

Ofisi ya Usalama wa Umma ya Beijing haikujibu lolote kuhusiana na tuhuma hizo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China,Zhao Lijian alionya waandamanaji na waandishi habari kuwa haki na uhuru lazima zitumike ndani ya mfumo wa sheria.

"Siku zote China inakaribisha waandishi wa habari wa kigeni kufanya shughuli za kuripoti nchini China kwa mujibu wa sheria na kanuni husika, na tumefanya mengi kuwezesha na kutoa urahisi wa kuripoti. Wakati huo huo, wakati wa kufanya shughuli za kuripoti nchini China, waandishi wa habari wa kigeni wanapaswa kufuata kwa uangalifu sheria na kanuni za China.'',alisema Lijian.

Ukuaji wa kiuchumi wafifia

Picha: Hector Retamal/AFP/Getty Images

Kutoridhika na sera za miaka mitatu ya vizuizi vikali vya COVID-19,maandamano yalipamba moto katika miji kadhaa ya China. Wimbi hili kubwa la uasi wa kiraia nchini China tangu Rais Xi Jinping achukuwe madaraka miaka kumi iliyopita,linakuja wakati idadi ya maambukizi ya COVID imeongezeka na sehemu  kadhaa za miji zinakabiliwa na vizuizi vipya. Afisa mmoja wa afya alisema malalamiko dhidi ya udhibiti wa COVID-19 yalikuwa hasa kuhusu utekelezaji wa masharti makali.

Virusi vya corona vimeenea licha ya China kujitenga kwa kiasi kikubwa na ulimwengu na kudai dhabihu muhimu kutoka kwa wanchi wake, kuzingatia upimaji wa mara kwa mara.

Uingiliaji kati wa kimataifa?

Ongezeko la vizuizi limezidisha kushuka kwa kasi zaidi ukuaji wa uchumi wa China  na kuvuruga minyororo ya ugavi ulimwenguni na kuporomoka kwa fedha  kwenye masoko. China imelaumu uingiliaji kati wa kimataifa katika maandamano yanayoendelea hivi sasa. Mara kwa mara mamlaka za China huonya kwamba nguvu za kigeni zinahatarisha usalama wa taifa na zimechutumu uchochezi wa maandamano ya 2019 ya kuunga mkono wanaharakati wa demokrasia Hong Kong.