1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroIsrael

Maafisa usalama wastaafu wa Israel waomba msaada wa Trump

4 Agosti 2025

Zaidi ya maafisa 600 wastaafu wa usalama nchini Israel wamemuomba Rais Donald Trump wa Marekani kuongeza shinikizo dhidi ya serikali yao ili kuvimaliza vita kwenye Ukanda wa Gaza.

Marekani Washington D.C. 2025 | Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani akizungumza kwenye bustani iliyopo Ikulu ya White HousePicha: Carlos Barria/REUTERS

Maafisa hao ambao ni pamoja na wakuu wa zamani wa mashirika ya intelijensia wamesema kwa tathmini yao ya kitaalamu, Gaza sio tishio tena kwa Israel.

Wamesema hayo kwenye barua ya wazi iliyotangazwa na vyombo va habari mapema leo, wakimuomba Trump kusimamia maamuzi ya Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na hasa kuhusiana na usitishwaji mapigano.

Mkurugenzi wa zamani wa Shirika la Usalama la Israel Ami Ayalon ameonya kwamba vita hivyo vinavyokaribia mwezi wa 23 vinaifanya Israel kudhoofika kiusalama na kupoteza utambulisho wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW