1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Hiroshoma yawataka viongozi kutoendeleza mgogoro wa nyuklia

6 Agosti 2024

Maafisa mjini Hiroshima nchini Japan wamewataka viongozi wa dunia kuacha kutumia silaha za nyuklia kama kigezo cha kuzua hofu na badala yake wachukuwe hatua mara moja kukomesha matumizi yake.

Japan | Hiroshima | Maadhimisho ya miaka 79 tangu shambulio la nyuklia.
Maadhimisho ya kumbukizi ya miaka 79 tangu kupigwa kwa bomu la nyuklia mji wa Heroshima JapanPicha: JAPAN POOL/JIJI Press/AFP/Getty Images

Hatua ambayo itaondoa uwezekano wa vita vya atomiki wakati ambapo migogoro inaendelea Ukraine na Mashariki ya Kati pamoja na mvutano katika eneo la Asia Mashariki.

Wameyasema hayo leo katika tukio la kumbukumbu ya miaka 79 tangu kufanyika shambulizi la bomu la atomiki kwenye mji huo wa Hiroshima mwishoni mwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. 

Soma pia:China imesitisha mazungumzo ya kudhibiti silaha na Marekani

Gavana wa Hiroshima Hidehiko Yuzaki amesema mataifa yenye silaha za nyuklia na wale wanaotumia silaha za nyuklia kama kitisho vitani, wapuuza kwa makusudi ukweli kwamba mara tu watu wanapovumbua silaha, wao huzitumia bila ubaguzi.

Yuzaki ameongeza kuwa maadamu silaha za nyuklia zipo, ni wazi zitatumika tena siku moja.

Takriban watu 50,000 waliohudhuria sherehe hiyo walikaa kimya kwa dakika moja na kengele ya amani ikapigwa mwendo wa saa mbili na robo asubuhi muda ambao ndege ya Marekani aina ya B-29 iliangusha bomu mjini humo mwka wa 1945.