1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa juu Marekani wasema uchaguzi ulikuwa salaama

13 Novemba 2020

Maafisa wa serikali za majimbo na shirikisho nchini Marekani wamesema hawana ushahidi wowote wa udaganyifu katika uchaguzi wa rais wa wiki iliyopita, wakitupilia mbali madai ya rais Donald Trump na washirika wake.

USA US Wahl 2020 Protest Trump-Anhänger Stop the Steal
Picha: James Atoa/UPI Photo/newscom/picture alliance

Taarifa ya maafisa wa serikali na sekta inayosimamia usalama wa uchaguzikwenye mtandao, imeutaja uchaguzi wa Novemba 3 kuwa uliokuwa na usalama zaidi katika historia ya Marekani.

Tamko lao linachukuliwa kama ukanushaji mkubwa zaidi wa moja kwa moja wa juhudi za Trump za kutilia mashaka uaminifu wa kinyang'anyiro hicho, na limerejea maelezo ya wataalamu wa uchaguzi na maafisa wa majimbo katika wiki iliyopita kwamba uchaguzi ulipita salaama bila kasoro kubwa.

Soma pia: Biden aendelea na mipango ya kuunda serikali

Katika taarifa hiyo iliyosambazwa na idara ya usalama wa mtandaoni na usalama wa miundombinu, maafisa hao walisema: "Wakati tunafahamu kuna madai mengi yasiyo na msingi na fursa za upotoshaji kuhusu mchakato wa uchaguzi wetu, tunaweza kuwahakikishia kwamba tuna imani ya juu kabisaa katika usalama na uaminifu wa uchaguzi wetu, na nyinyi mnapaswa kuwa imani pia."

Wafuasi wa Trump wakiwa kwenye mkutano kupinga kile wanachokiita wizi wa kura, mjini Las Vegas, Novemba 8, 2020.Picha: James Atoa/UPI Photo/newscom/picture alliance

Mkurugenzi wa idara hiyo ambayo iliyoongoza juhudi za kuulinda uchaguzi wa shirikisho Chris Krebs, aliripotiwa mapema na shirika la habari la Reuters kwamba aliwambia washirika wake kuwa anatarajia kufutwa kazi na rais Trump. Krebs amekuwa akipaza sauti kupitia mtandao wa Twitter kuwahakikishia Wamarekani kwamba uchaguzi ulikuwa salaama na kwamba kura zao zote zitahesabiwa.

Soma pia:Maoni: Matarajio ya Afrika kwa Marekani

Tamko lapuuza malalamko ya Trump

Waandishi wa tamko hilo wamesema hawana ushahidi kwamba mfumo wowote wa uchaguzi ulifuta au kupoteza kura, kubadilisha kura, au kuhatarishwa kwa namna yoyote. Wamesema majimbo yote yalio na matokeo yanayokaribiana yana rekodi za karatasi, zinazoruhusu kuhesabiwa tena kwa kila kura iwapo hilo linahitajika, na kwa ajili ya utambuzi na urekebishaji wa makosa yoyote yale.

Soma pia: Ushindi wa Joe Biden: Huruma imeshinda urais

Masuala yanayoibuliwa na kampeni ya Trump na washirika wake ni yale yanyojitokeza katika chaguzi zote, ambayo ni matatizo ya sahihi, bahasha za siri na alama za posta kwenye kura zinazotumwa kwa njia ya posta, pamoja na uwezekano wa idadi ndogo ya kura kupigwa vibaya au kuoptea. Wakati Mdemocrat Joe Biden akiongoza mbele ya Trump katika majimbo ya maamuzi, hakuna kati ya masuala hayo litakalokuwa na athari kwenye matokeo ya uchaguzi.

Rais mteule wa Marekani Joe Biden.Picha: Biden Campaign/RS/MPI/Capital Pictures/picture alliance

Soma pia:Trump awazuia wafanyikazi wa Ikulu kutoa ushirikiano kwa Biden

Wakati huo huo, salaam za pongezi zimeendelea kumiminika kwa rais mteule Joe Biden, ztikiwemo kutoka kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis na serikali ya China, ambayo awali ilisita kumpongeza Biden. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Wanga Wenbin, amesema katika mkutano wa kawaida wa waandishi habari, kwamba wanaheshimu chaguo la Wamarekani, na kutoa pongezi kwa Biden na makamu wake mteuele Kamala Harris.

Republican waanza kukubali ukweli

Huku hayo yakijiri, idadi inayoongezeka ya wabunge wa chama cha Republican, wameutolea mwito utawala rais Trump kuacha kumuzuia Biden kupata taarifa za kiusalama, katika kile kinachoelezwa kuwa utambuzi wa kimya kimya kwamba Biden ataingia ikulu ya White House muda si mrefu licha ya Trump kuendelea kukata kukubali kwamba ameshindwa.

Biden azidi kupongezwa kwa ushindi licha ya Trump kukataa kukubali kushindwa

01:06

This browser does not support the video element.

Maafisa wengi wa Republican na wabunge wamekuwa wanaunga mkono wazi juhudi za Trump za kubadilisha matokeo ya uchaguzi kupitia mkururo wa kesi za kisheria katika majimbo tofauti, kufuatia madai ya rais yasio na msingi juu ya udanganyifu mkubwa wa uchaguzi.

Soma zaidi: Biden azidi kupongezwa

Maseneta wa Republican wakiwemo John Cornyn, Ron Johnson, Chuck Grassley na Lindsay Graham siku ya Alhamisi waliusihi utawala wa Trump kumruhusu Biden kupata taarifa za kila siku za rais kuhusu hali ya usalama.

Kawaida marais wateule hupokea taarifa kama hizo kutoka mashirika ya upelelezi, kujifunza juu ya vitisho vinavyoikabili Marekani kabla ya kuingia madarakani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW