1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaAsia

Maafisa wa Korea Kusini wataka Rais Yoon Suk Yeol akamatwe

30 Desemba 2024

Maafisa wa Korea Kusini wameomba kibali cha kukamatwa kwa rais aliyesimamishwa kazi Yoon Suk Yeol, shirika la habari la nchini humo la Yonhap limeripoti mapema leo Jumatatu.

Südkorea Martial Law Protest
Washiriki wakishangilia baada ya kusikia habari kwamba bunge la Korea Kusini lilipiga kura ya kumuondoa Rais Yoon Suk Yeol nje ya Bunge la Seoul, Korea Kusini, Jumamosi, Desemba 14, 2024.Picha: Lee Jin-man/AP/picture alliance

Ofisi ya Uchunguzi wa Ufisadi inamchunguza Yoon baada ya kutangaza amri ya kuiweka nchi chini ya sheria ya kijeshi mnamo Desemba 3. Ofisi hiyo ilisema kwamba Yoon pia alikuwa amepuuza hati tatu za kuitwa mahakamani kwa ajili ya kuhojiwa. Korea Kusini imekuwa katika mzozo wa kisiasa tangu wakati huo.Bunge la kitaifa lilipiga kura ya kumshtaki Yoon mnamo Desemba 14, na kwa sasa mahakama ya katiba imeanzisha taratibu husika ili kutoa uamuzi wa mwisho kuhusu iwapo kura ya bunge ni ya kikatiba au la. Choi Sang Mok sasa anakaimu urais tangu Ijumaa iliyopita baada ya wabunge kupiga kura ya kumuondoa Han Duck Soo aliyekuwa anakaimu nafasi hiyo baada ya Yoon kuondolewa kwenye kiti cha urais.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW