Wajumbe wa Pakistan na Afghanistan kukutana Doha
18 Oktoba 2025
Maafisa wa Pakistan watafanya mazungumzo hii leo Jumamosi na wenzao wa Afghanistan huko Qatar, ikiwa ni siku moja baada ya Islamabad kufanya mashambulizi ya angani dhidi ya jirani yake. Mashambulizi hayo yamewaua watu 10 na kuvunja makubaliano ya usitishaji mapigano ambayo yalileta utulivu kwa siku mbili katika eneo la mpaka.
Waziri wa ulinzi Khawaja Asif na Mkuu wa ujasusi Asim Malik wanaongoza ujumbe wa Pakistan katika mazungumzo hayo. Serikali ya Afghanistan chini ya Taliban nayo imesema ujumbe wa ngazi ya juu wa nchi hiyo ukiongozwa na waziri wa ulinzi Mohammed Yaqub, unaelekea Doha tayari kwa mazungumzo.
Makubaliano ya masaa 48 ya usitishaji mapigano yalituliza wiki moja ya makabiliano makali ya mpakani ambayo yameua dazeni ya wanajeshi na raia kutoka kila upande.