1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa wa Sweden na Uturuki kukutana mjini Brussels

6 Julai 2023

Maafisa wa Sweden na Uturuki wanakutana katika makao makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Brussels nchini Ubelgiji, kujadili masharti ya Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan kwa Sweden kujiunga na muungano huo.

NATO Headquarter Brüssel
Picha: Geert Vanden Wijngaert/ASSOCIATED PRESS/picture alliance

Maafisa wa Sweden na Uturuki watakutana leo katika makao makuu ya Jumuiya ya Kujihami ya NATO mjini Brussels nchini Ubelgiji, ili kujadili hatua za Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan za kuizuia Sweden kujiunga na muungano huo wa kijeshi.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami ya NATO Jens Stoltenberg atauongoza mkutano huo ambao utawaleta pamoja mawaziri wa mambo ya nje, wakuu wa ujasusi na washauri wa kitaifa wa usalama wa nchi husika ili kutathmini iwapo kuna hatua zinazoweza kuchukuliwa kuelekea mwafaka.

Uturuki na Hungary ndizo zimeizuia Sweden kuwa mwanachama wa jumuiya ya NATO wakati wanachama wengine 29 wamesema Sweden imechukua hatua za kutosha kuyatimiza masharti ya Uturuki.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW