1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Maafisa wa UN waonya kuongezeka kwa mateso ya raia wa Sudan

3 Novemba 2023

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameonya kuhusu kuongezeka kwa mateso ya raia wa Sudan wakati kukishuhudiwa mapigano makali huko Darfur ambayo yamesababisha kwa mara nyingine maelfu ya raia kuyahama makazi yao.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu, mzozo kati ya jeshi na kundi la RSF nchini Sudan tayari umesababisha pia vifo vya watu 9,000. na maelfu wamekimbilia nchi jirani.
Tangu mwezi Aprili mwaka huu, mzozo kati ya jeshi na kundi la RSF nchini Sudan tayari umesababisha pia vifo vya watu 9,000. na maelfu wamekimbilia nchi jirani.Picha: Blaise Dariustone/DW

Mamadou Dian Balde, afisa mkuu wa kikanda wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) amesema ni mateso ya kutisha kuona miezi sita ya mzozo Sudan, na tayari watu 6,000,000 wamelazimishwa kuyahama makazi yao, ikiwa ni wastani wa milioni moja kwa mwezi.

Mnamo Alhamisi, afisa mwingine wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo, Dominique Hyde, alisema ameshuhudia "hali ya kutisha" kwenye mpaka na Sudan ambapo karibu watu 10,000 waliokimbia vurugu wamewasili katika siku tatu zilizopita.

Tangu mwezi Aprili mwaka huu, mzozo kati ya jeshi na kundi la RSF nchini Sudan tayari umesababisha pia vifo vya watu 9,000.