1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Ukaraine yaishambulia meli ya ya mafuta ya Urusi.

5 Agosti 2023

Urusi imesema meli yake ya mafuta imeshambuliwa na ndege isiyo na rubani ya Ukraine kwenye mlango wa Kerch katika jimbo la Crimea.

Russland Noworossiysk Öltanker im Hafen
Picha: Vitaly Timkiv/SNA/IMAGO

Maafisa wa Urusi wameripoti kwamba meli yao ya mafuta imeshambuliwa na ndege isiyo na rubani kwenye mlango wa Kerch katika jimbo la Crimea. Hujuma hiyo imefanyika siku moja baada ya meli ya kivita kushambuliwa karibu na daraja la Kerch. Hatua za tahadhari zilichukuliwa kwa kuifunga sehemu ya daraja hilo kwa muda wa saa tatu. Shirika la habari la Urusi Tass, limeripoti kwamba waokoaji wa baharini walipelekwa katika bandari ya Bahari Nyeusi kusaidia kuihamisha meli hiyo. Shirika hilo la habari limesema hakuna mafuta yaliyomwagika kutoka kwenye meli hiyo iliyokuwa na wafanyakazi 11. Urusi na Ukraine zimeongeza mashambulizi kwa kutumia ndege zisizo na rubani kwenye bahari Nyeusi baada ya Urusi kujiondoa kwenye makubaliano ya usafirishaji wa nafaka mwezi uliopita.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW