1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAmerika ya Kaskazini

Maafisa wa usalama Minneapolis waagizwa kuvaa camera kazini

3 Februari 2026

Waziri wa Usalama wa Ndani nchini Marekani Kristi Noem ametangaza kwamba kila afisa wa Usalama wa Shirikisho aliyeko Minneapolis atalazimika kuvaa camera. Maafisa hao ni pamoja na wa uhamiaji na wa Forodha, ICE.

Marekani Minneapolis 2026 | Waandamanaji na watazamaji katika maandamano ya kupinga uvamizi wa maafisa wa ICE
Watu wakiwatazama waandamanaji wakati wa maandamano dhidi ya utekelezaji wa sheria za ICE mnamo Januari 30, 2026 huko Minneapolis, Minnesota.Picha: Stephen Maturen/Getty Images

Uamuzi huo unatolewa katikati ya maandamano yaliyosambaa pamoja ukosoaji baada ya kisa cha raia wa Marekani kuuliwa na maafisa wa uhamiaji katika mji huo wa Minneapolis

Rais Donald Trump, ambaye alibatilisha agizo kama hilo lililotolewa na mtangulizi wake Joe Biden ameonekana kuunga mkono uamuzi wa Noem alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Washington.

Amesema "Haikuwa uamuzi wangu. Ningemwachia, unajua, hilo. Kwa ujumla camrea huwa ni kwa watekezaji wa sheria kwa sababu hawawezi kudanganya kuhusu kinachoendelea. Kwa hivyo, kwa ujumla, nadhani kwa asilimia 80 ni hatua nzuri kwa vyombo vya sheria. Na ikiwa anataka kufanya hivyo, nakubaliana nalo. Kumbuka jambo moja, tulifunga mpaka. Nilichaguliwa wakati kuna hali mbaya mpakani, lakini sasa hakuna anayeingia kupitia mpaka wetu tena."

Noem ameahidi uamuzi huo kutekelezwa kote nchini humo baada ya fedha kupatikana.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW