SiasaSenegal
Raia nchini Senegal wapiga kura kumchagua rais mpya
24 Machi 2024Matangazo
Karibu watu milioni 7.3 wameandikishwa kupiga kura katika taifa hilo la Afrika Magharibi ambapo wagombea wawili wanaopigiwa upatu, Waziri Mkuu wa zamani wa muungano unaotawala, Amadou Ba na Bassirou Diomaye Faye wa upinzani wakichuana vikali.
Mshindi atakuwa na jukumu la kuiongoza Senegal kutoka kwenye changamoto zilizoshuhudiwa hivi karibuni na kusimamia mapato yatokanayo na akiba ya mafuta na gesi ambayo yataanza kuzalishwa hivi karibuni.
Vituo vya kura vinatarajiwa kufungwa saa 12.00 za jioni kwa majira ya nchini humo na matokeo rasmi yakitarajiwa kutolewa wiki ijayo.