1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maafisa watatu wa Liberia waachishwa kazi kwa ufisadi

1 Novemba 2024

Rais wa Liberia Joseph Boakai, amewaachisha kazi maafisa watatu waandamizi kutoka taasisi inayoshughulikia kurejea kwa wakimbizi kuhusiana na tuhuma za ufisadi na ubadhifiru wa fedha.

Rais wa Liberia Joseph Boakai
Rais wa Liberia Joseph BoakaiPicha: Pulloh Moh-Marsi/Matrix Images/picture alliance

Rais wa Liberia Joseph Boakai, amewaachisha kazi maafisa watatu waandamizi kutoka taasisi inayoshughulikia kurejea kwa wakimbizi kuhusiana na tuhuma za ufisadi na ubadhifiru wa fedha. Tume ya Liberia ya Kuwarejesha na Kuwapa Makazi Wakimbizi - LRRRC katika miezi ya karibuni imeshughulikia kurejea nyumbani kwa zaidi ya Waliberia 1,000 waliokimbia vita vikali vya wenyewe kwa wenyewe.

Wengine zaidi ya 2,500 wanatarajiwa kurejeshwa ifikapo mwisho wa mwaka huu. Wengi walikimbilia nchi jirani za Afrika Magharibi, ikiwemo Cote d'Ivoire, Guinea, Sierra Leone na Ghana.Rais wa Liberia yuko tayari kupunguza mshahara wake kwa asilimia 40

Ofisi ya Rais imesema katika taarifa kuwa Mkurugenzi Mkuu Patrick Worzie, Naibu Mkurugenzi wa Operesheni Richard Hoff na Naibu Mkurugenzi wa Utawala AJ Armah Karneh wamesimamishwa kazi mara moja.

Tume ya kupambana na rushwa itafanya uchunguzi. Mfichua siri alitoa nyaraka zilizodaiwa kuonyesha dosari katika matumizi ya karibu dola milioni 1.5. Rais Boakai, aliyeanza muhula wake wa miaka sita mwezi Juanuari, ameahidi kupambana na ufisadi uliokithiri nchini Liberia, moja ya nchi maskini zaidi duniani.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW