1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya COVID-19 bado yaongezeka duniani

Sekione Kitojo
22 Juni 2020

Dunia imeshuhudia ongezeko kubwa  zaidi la siku moja kuwahi kutokea katika katika maambukizi ya virusi vya corona, ambapo maambukizi yamepanda katika vijiji nchini India, baada ya wafanyakazi kuikimbia miji mkubwa.

Indien Wanderarbeiter verlassen Neu Delhi wegen der Corona Pandemie
Picha: Reuters/A. Abidi

Wakati  huo huo mataifa ya Ulaya yanafurhia ulegezwaji wa taratibu wa hatua za kuwazuwia watu kusalia majumbani mwao lakini katika mahospitali  mataifa hayo yanajitayarisha  kwa  wimbi  la  pili la maambukizi.

Wafanyakazi walioahamia mijini wakijitayarisha kurejea vijijini kwao nchini India. Hali inayosababisha maambukizi vijijini.Picha: Reuters/A. Abidi

Idadi ya maambukizi  nchini India  imepanda  kwa  karibu  watu 15,000 hadi hii  leo Jumatatu na  kufikia  kesi 425,282, ambapo watu zaidi  ya  13,000 wamefariki, wizara  ya  afya  imeripoti.

Baada ya kulegeza  hatua za kuwazuwia  watu kusalia  majumbani mwao, serikali ya  India  imetumia  treni  maalum  kuwarejesha maelfu ya  wafanyakazi  wahamiaji  kwenda  katika  vijiji  vyao katika wiki  za  hivi  karibuni.

Karibu asilimia 90 ya  wilaya  masikini  nchini  India  zina kesi  za maambukizi, licha  ya  kuwa  maambukizi  zaidi  yanabakia  kuwa Delhi, Maharashtra, na  Tamil Nadu, majimbo ambayo yana  miji mikubwa. Maambukizi  yamepungua  nchini  China  na  Korea  kusini, ikionesha  hatua  za  maendeleo katika  kudhibiti mripuko  mpya. Lakini  licha  ya  hatua  hizo  katika  kudhibiti  virusi  hivyo  katika kanda  ambazo ziliathirika mapema  kutokana  na  kuzuka  kwa  virusi hivyo, dunani  kwa  jumla  idadi ya  kesi  za  maambukizi  mapya imepanda  katika  siku  za  hivi  karibuni.

Wahudumu katika mahospitali wakipata maelezo kutoka kwa viongozi mjini MoscowPicha: picture-alliance/AP/Mayor Press Service/D. Grishkin

Mahospitali yanapata shinikizo kuwahudumia wagonjwa

Nchini  Brazil, Iraq, India  na  Marekani, mahospitali  yamefikia katika  hatua  ya  kushindwa  kuwahudumia  wagonjwa.

Karibu  watu  milioni 9 wameambukizwa  na  virusi  vya  corona na zaidi ya  watu 468,000 wamefariki, kwa  mujibu wa idadi  iliyowekwa pamoja  na  chuo kikuu  cha Johns Hopkins. Wataalamu  wanasema idadi  halisi  ni ya juu  zaidi, kutokana  na  ukomo  wa  kufanya uchunguzi  pamoja  na  kile  kinachofikiriwa  kuwa  ni idadi  kubwa  ya watu  ambao  hawaoneshi  dalili.

Idadi ya kesi zilizothibitishwa  nchini  Ujerumani  imepanda kwa  watu 537  hadi  watu 190,359, ikiwa  ni  data  kutoka  taasisi  ya  Robert Koch ya  kudhibiti  magonjwa  ya  maambukizi zimeonesha  leo Jumatatu.

Idadi  ya  watu  waliofariki  imeongezeka  kwa  watu watatu, na kufikia  watu 8,885.

Kampuni ya machinjio ya Toennies nchini Ujerumani ambayo wafanyakazi wake wameambukizwa na virusi vya corona..Picha: picture-alliance/dpa/G. Kirchner

Idadi ya kesi zilizothibitishwa  katika  machinjio nchini  Ujerumani imepanda  kwa  watu 300 jana, hadi  watu 1,331, wakati maafisa kutoka  katika  jimbo  la  North Rhine Westfalia  wakifanya  ziara katika  eneo  hilo  ambalo limezusha  hofu ya  wimbi  la  pili la maambukizi. Maafisa  walikuwa  wanasubiri matokeo  ya  uchunguzi wa  kiasi  ya watu 250  kutoka  idadi  ya  watu 6,139  ambao umekwisha  fanyika  katika  kampuni  hiyo  ya  machinjio.

Italia imeripoti  vifo vipya 24  kutokana  na  ugonjwa  wa  COVID-19 jana, ikiwa  ni  kiwango  cha  chini cha vifo vya  kila  tangu Machi 2, mnamo wakati  vifo  vya watu 18 viliripotiwa.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW