1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya COVID-19 yapindukia milioni 250

9 Novemba 2021

Maambukizi ya corona duniani imepindukia milioni 250 huku bara la ulaya likirekodi idadi kubwa zaidi ya maambukizo ikifuatiwa na Asia.

Ukraine Symbolbild Covid-19 Coronavirus
Picha: Photoshot/picture alliance

Kulingana na takwimu kutoka Chuo Kikuu cha John Hopkins cha nchini Marekani zaidi ya watu milioni 250 duniani wameambukizwa  Corona na zaidi ya milioni 5 wameaga dunia kutokana janga hilo. Ulaya imesajili zaidi ya visa milioni 76 vya maambukizo ya COVID-19.

Ikifuatiwa na Asia, ikiwa na visa zaidi ya milioni 56, Marekani na Canada zilizo na kesi zaidi ya milioni 48, wakati Amerika ya Kusini na Caribik zikiweka rekodi ya zaidi ya visa milioni 46. Katika siku saba zilizopita, kumesajiliwa karibu maambukizo mapya laki 4,49 kila siku.

Soma Zaidi: Ujerumani yakaza sheria dhidi ya COVID-19

Ongezeko hili linajiri wakati nchi zinalegeza vikwazo vya biashara na usafiri na idadi inaendelea kupanda katika mataifa ya Ulaya mashariki

Ujerumani yakabiliwa na maambukizi mengi.

Taasisi ya kudhibiti magonjwa ya Ujerumani ya Robert Koch iliripoti idadi ya maambukizo mapya kwa kila wakaazi laki 1 katika siku saba zilizopita kuwa 213.7, hii ikiwa mara ya kwanza kiwango hicho kupita 200 tangu janga hilo kuanza.

Wataalamu wa afya wanasema kuwa idadi ya vifo vinavyotokana na Corona imepungua nchini Ujerumani kutokana na theluthi mbili ya watu kupata chanjo kamili.

Idadi a vifo imepungua kutokana na utoaji wa chanjo unaoendeleaPicha: Andriy Andriyenko/Zumapress/picture alliance

Hata hivyo Profesa Schönrich kutoka hospitali ya Charite iliyoko mjini Berlin aliiambia DW kwamba hii haitoshi na kwamba hali inazidi kuwa mbaya katika hospitali za Ujerumani.

"Kwa namna fulani tumewafikia watu ambao hawajachanjwa na kuwashawishi kwamba wanapaswa kuchanjwa. Na chanjo hiyo ina maana ya ulinzi wao wenyewe, lakini pia ulinzi kwa wenzao. Hiyo ni hatua muhimu sana. Na bila hiyo, nadhani hatutaweza kulizuia wimbi la nne." alisema Profesa Schnrich.

Matumizi ya pasi ya afya huenda yakaanza upya Denmark.

Waziri mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen amesema wataanzisha tena matumizi ya pasi ya afya katika huku kukiwa na ongezeko kubwa la maambukizi ya COVID-19.

Urusi iliripoti rekodi ya vifo 1,211, siku ya Jumanne, siku moja tu baada ya kuondolewa marufuku ya kufungwa kwa maeneo ya kazi nchini kote kwa lengo la kudhibiti maambukizi.

Soma Zaidi:Ujerumani yaomboleza watu 80,000 waliokufa kwa Corona

Nchini Marekani, mahakama ya Texas imepitisha uamuzi wa kuliunga mkono  shirika la ndege la United Airlines kwa kuwaweka wafanyakazi wake wanaokataa kuchanjwa kwa misingi ya kidini na kimatibabu  katika  likizo bila malipo.

Hii leo maelfu ya watu wameandamana mjini Wellingtone mji mkuu wa New Zealand, kuelekea bungeni kupinga vizuizi vilivyowekwa kuzuia kusambaa maambukizo ya COVID-19. Singapore imetangaza mipango ya kuwataka wagonjwa ambao hawajachanjwa wajilipie gharama zao za matibabu kuanzia mwezi ujao.

Mashirika: https://p.dw.com/p/42l98

Ruka sehemu inayofuata Gundua zaidi
Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW