1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya Omicron Afrika Kusini huenda yamefikia kilele

20 Desemba 2021

Visa vya hivi karibuni vya maambukizi ya virusi vya Corona nchini Afrika Kusini vinaonesha kwamba kitovu cha mripuko wa hivi karibuni uliochochewa na aina mpya ya virusi hivyo,Omicron huenda ukafikia kilele chake.

Neue COVID-19-Variante Omicron
Picha: Pavlo Gonchar/Zumapress/picture alliance

Katika mkoa wa Gauteng ambako ndiko kulikogunduliwa visa vya mwanzo vya maambukizi ya virusi hivyo, kumeripotiwa visa vipya 3,582 vya maambukizi katika kipindi cha saa 24 zilizopita siku ya Jumatatu.

Kiwango hicho kimepungua ikilinganishwa na hali ilivyokuwa wiki iliyopita ambapo visa 7,488 viliripotiwa katika muda sawa na huo.

Tathmini hiyo imetolewa na taasisi ya kitaifa inayohusika na magonjwa ya kuambukiza NICD.

Kiwango cha juu zaidi cha maambukizi kilichoripotiwa jana Jumapili ni 4,135 kutokea mkoa wa mashariki wa Kwazulu Natal ambako shughuli za kitalii zimeongezeka wiki iliyopita katika eneo lake la pwani.