1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi ya virusi vya corona yapindukia watu milioni 3

28 Aprili 2020

Rekodi mpya visa vya maambuziki ya virusi vya corona hadi sasa inaonesha vimepindukia watu milioni tatu  duniani kote, ambapo karibu asilimia 80 vimerekodiwa Ulaya na Marekani.

Äthiopien Addis Ababa | Coronavirus | Video Anruf aus Wuhan
Picha: imago images/Xinhua

Wakati hali ikiwa hivyo, Umoja wa Mataifa ukisema kunahitajika kitita cha kiasi cha dola bilioni 90 ili kunusuru jumla ya watu milioni 700 walioathirika zaidi wakiwemo wa katika maeneo masikini, ambayo kilele cha maambukizi hayo bado hakijafikia.

Kwa takwimu za shirika la habari la AFP  takribani maambukizi 3,003,344 yamebainika, ikiwemo vifo 209,388, na vingi vya hivyo vimetokea Ulaya ambako kuna jumla ya maambukizi 1,393,779 na vifo 126,233. Marekani kuna maambukizi 980,008 vikiwemo vifo 55,637.  Mkuu wa ofisi ya misaada ya kibinaadamu ya Umoja wa Mataifa Mark Lowcock amesema kiasi hicho cha dola bilioni 90 ambaco amependekeza kitolewe kwa masharti nafuu kinaweza kusaidia katika kuongeza kipato, chakula na afya kwa  jamii ya takribani watu 700 iliyo katika hatari zaidi.

Mratibu wa misaada ya kiutu wa UN Mark LowcockPicha: picture-alliance/Keystone/S. Di Nolfi

Mashiriki ya kimataifa kuwa wafadhili wakuu

Amesema pamoja na wafadhili wengine  theluthi mbili za kiasi hicho cha bilioni 90 kitatolewa na taasisi za kifedha za kimataifa kama Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani IMF. Katika taarifa yake kwa njia ya video alisema kilele cha COVID-19 hakijafika katika katika maeneo masikini zaidi lakini alikiwa hali inaweza kuwa tofauti katika kipindi cha wiki miezi mitatu hadi sita toka sasa. Na katika hatua nyingine Rais Donald Trump wa Marekani ameilaumu China kwa kusema taifa hilo lingweza kudhibiti kusambaa kwa virusu vya corona kabla havijavuta mipaka ya taifa hilo. Kutokana na hali hiyo anasema serikali yake imeanzisha uchunguzi makini wa kile kilichotokea.

Wagonjwa 12 wa mwisho wa Wuhan watolewa hospitali

Wahudumu wa afya wa Wuhan wakimsaidia mgonjwaPicha: picture-alliance/dpa/F. Maohua

Na ndani ya Chinana hasa katika mji wa Wuhan ambao ndio kitovu cha mripuko wa virusi vya corona kunatajwa kutokwepo tena kwa mgonjwa alielazwa hospitali baada ya wagonjwa 12 wa mwisho kuruhusiwa kurejea nyumbani. Ikumbekwe katika mji huo takribani watu 3,869 walithibitika kufa na kufanya jumla ya asilimia 80 ya vifo vyote nchini humo. Hata hivyo kamisheni ya afya ya jimbo hilo imesema pamoja na kutokuwepo kwa kesi ya wanaohisiwa kuwa na virusi vya corona katika hospitali, lakini watu 1, 728 ambao walikuwa na maingiliano na waliaombukizwa watasalia katika uangalizi wa kimatibabu. Wagonjwa wameendelea kuhudumiwa katika mahospitali katika maeneo tofauti ya China wakiwemo 67 Shanghai na watatu Beijing.

Kwa upande mwingine Kiongozi wa Hong Kong Carrie Lam amesema idadi kubwa ya watumishi wa umma wanatarajiwa kurejea katika majukumu yao ya kazi kuanzia Mei 4. Hata hivyo serikali bado haijtoa uamuzi wa kuondosha vikwazo vya kusafiri na vingine vya kujongeleana ambavyo vinatarajiwa kufikia kikomo chake wiki ijayo. Ikiwa kama ilivyo katika maeneo mengine ya ulimwengu katika kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya corona Hong Kong ilifunga shule, watu wengi walifanya kazi kutoka nyumbani na imekuwa sio jambo rahisi kuwaona watu wakitembea pasipo kuvaa barakoa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW