1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizi yapindukia milioni 1 Marekani

29 Aprili 2020

Idadi ya maambukizi nchini Marekani imepindukiwa watu milioni moja katika kipindi ambacho Ufaransa imetangaza kupunguza masharti ya kukabiliana na kasi ya kusambaa kwa virusi vya corona kuanzia Mei 11.

USA Detroit | Coronavirus | Passanten mit Mundschutz
Picha: Reuters/S. Stapleton

Nchini Marekani wakati idadi ya vifo, vilivyotokana na ugonjwa wa COVID-19 inapindikia watu 58,000, ikiwa ni zaidi ya wale waliouwawa katika Vita ya Vietnam, pamoja na mambo mengine rais Donald Trump wa taifa hilo amesema serikali inafikira kuanzisha mpango wa kuwapia abiria katika viwanja vya ndege na hasa kwa wale wanaotoka katika maeneo yaliathirika zaidi.

Kwa mujibu wa takwimu za shirika la habari la Uingereza idadi ya vifo nchini Marekani imeongezeka mara mbili zaidi katika kipindi cha siku 18. Na hivyo kulifanya taifa hilo kuwa na theluthi moja ya maambukizi yote duniani. Hata hivyo Trump amesaini amri ya kutaka viwanda vya usindikaji nyama kuendelea na kazi zake pamoja na kukosolewa kwa kuhatarisha maambukizi kwa wafanyakazi wa sekta hiyo. Hata hiyo Trump amesisita msimamo wake wa kudai itawasaida Wamarekani kupata chakula cha kutosha.

Rais Emmanuel Macron wa UfaransaPicha: Reuters/Pool/Y. Valat

Ufaransa kupunguza masharti Mei 11.

Kwa upande mwingine Ufaransa imeuweka wazi mpango wake wa kupunguza masharti ya kukabiliana na janga la coronakuanzia Mei 11, ambapo pamoja na mambo mengine uvaaji wa barakoa utakuwa jambo la lazima katika usafiri wa umma. Vigezo vikali viliwekwa Machi 17, kwa shabaha ya kudhibiti virusi vya corona nchini humo. Rais Emmanuel Macron ameshatangaza kuondosha baadhi ya masharti kuanzia Mei 11, ingawa taarifa chache ndizo ziliwekwa wazi katika kipindi hiki.

Waziri Mkuu wa Ufaransa, Edourd Philipppe amesema masharti ya kuendelea kutenga nafasi kati ya mtu mmoja na mwingine katika usafiri wa umma pia yataendelea kuwa ya lazima na pia kuwataka raia kuendelea na utaratibu wa kufanya kazi kutoka nyumbani. Ufaransa ni moja kati ya mataifa yaliathiriwa vibaya likiwa na rekodi ya maambukizi  watu zaidi 23,000.

Mkutano mkuu wa mwaka wa bunge la China kufanyika Mei 22.

Bunge la kitaifa la Jamhuri ya watu wa ChinaPicha: picture-alliance/Xinhua News Agency/Li Tao

Na serikali ya China imeamua kufanya mkutano wake mkuu wa bunge baada ya kuahirishwa kwa wiki kadhaa kutokana na mripuko wa janga la virusi vya corona. Mkutano huo ambao unaashiria kujiamini kwa China katika kufanikisha vita yake dhidi ya maradhi ambayo yalianza katika ardhi ya taifa hilo utafunguliwa May 22 mjini Beijing ambapo utajumuisha washiriki 3,000.

Kwa upande wa Afrika Rais Arthur Peter Mutharika wa Malawi amesema taifa lake litazindua mradi wa dharura wa kusafirisha fedha ambao utawahusu watu milioni moja pamoja na wafanyabiashara wadogo waliathiriwa na janga la corona. Kwa kupitia mpango huo kaya zinazostahili zitapokea kiasi cha kwacha elfu 35 fedha ya Malawi, ikiwa sawa na dola 40 kwa mwezi, ikilinganishwa na kiwango cha chini kabisa cha mshahara nchini humo.