1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maambukizo ya Uviko-19 yaripotiwa Kisumu, Kenya

7 Juni 2023

Wizara ya afya jimbo la Kisumu nchini Kenya imeripoti maambukizi ya ugonjwa wa Uviko-19 na homa ya mafua miongoni mwa wanafunzi huku shule takriban 5 zikiwa zimeaathirika zaidi.

Das Leben in ehemaligen Pandemie-Hotspots heute
Picha: DW

Kaimu mkurugenzi wa afya ya umma wa jimbo hilo Lilian Dayo amesema miongoni mwa wanafunzi 7 waliofanyiwa vipimo wiki iliyopita katika eneo bunge la Seme, huko Kisumu, 4 walipatikana na maambukizo ya Uviko- 19.

Baadhi ya shule zimewaagiza wanafunzi kuvaa barakoa ili kudhibiti maambukizi zaidi huku wakuu wa shule wakishauriwa kuwaruhusu wanafunzi walio na dalili za maambukizo kusalia nyumbani,.

Kwa sasa, wizara ya afya inahimiza kuzingatiwa kwa zoezi la kutolewa kwa chanjo dhidi ya Uviko-19 ikiwa ni pamoja na kukamilisha awamu zote na kuchomwa chanjo ya nyongeza.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW