1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroAfrika

Maandamano baada ya uchaguzi yaendelea Tanzania

30 Oktoba 2025

Polisi jijini Dar es Salaam nchini Tanzania wamewafyatulia risasi na mabomu ya machozi waandamanaji waliorejea barabarani Alhamisi katika siku ya pili ya maandamano.

Polisi wakikabiliana na raia jijini Dar es salaam 24.04.2025
Dar es salaam, TanzaniaPicha: Emmanuel Herman/REUTERS

 Baadhi ya maeneo ya mji huo yaliyoshuhudia mwendelezo wa maandamano Alhamisi ni pamoja na Mbagala, Gongo la Mboto na Kiluvya kulingana na watu walioshuhudia.

Raia wa Tanzania waliianza kuingia barabarani jijini Dar es salaam na katika miji mingine kutokana na kile kinachotajwa kuwa ukandamizaji mkubwa dhidi ya upinzani na wakosoaji wa serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan.

Amri ya kutokutoka nje yatangazwa

Jana Jumatano, polisi nchini humo walitangaza marufuku ya kutokutoka nje kuanzia saa kumi na mbili jioni wakati ambapo huduma ya intaneti imezuiwa. Watumishi wa umma na wanafunzi wameamriwa pia kubaki nyumbani Alhamisi kutokana na ghasia zinazoendelea.