1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maandamano dhidi ya Mubarak yaendelea Misri

Martin,Prema/ZPR5 Februari 2011

Mara nyingine tena, mamia kwa maelfu ya watu wameandamana katika mji mkuu wa Misri Cairo kupinga utawala wa Rais Hosni Mubarak alie madarakani kwa miaka 30.

Anti-government protestors camp in Tahrir Square, Cairo, Egypt, Saturday, Feb. 5, 2011. Rallies in Cairo and behind-the-scenes diplomacy from the Obama administration is piling more pressure on Egyptian President Hosni Mubarak to make a swift exit and allow a temporary government to embark on an immediate path toward democracy. (AP Photo/Manoocher Deghati)
Wapinzani wa Mubarak wapiga kambi mjini CairoPicha: AP

Wakipuuza amri ya kutotoka nje, waandamanaji hao walikusanyika kwenye uwanja wa Tahrir katikati ya Cairo.Wamesema wataendelea na maandamano hayo mpaka Rais Mubarak atakapon'gatuka madarakani.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Amr MussaPicha: AP

Hata Katibu Mkuu wa jumuiya ya nchi za Kiarabu, Amr Mussa alishiriki katika maandamano ya kumshinikiza Mubarak kujiuzulu yaliyoitwa "Siku ya Kuondoka". Mussa aliewahi kuwa waziri wa mambo ya nje katika serikali ya Mubarak, huenda akawa mmojawapo wa wagombea urais, baada ya kuondoka kwa Mubarak. Maandamano yalifanyika pia katika miji ya kaskazini, Alexandria na Port Said.

Wakati huo huo, Rais wa Marekani Barack Obama amesema, umma wa Misri umeeleza waziwazi kuwa unataka kuona mageuzi yanaanza sasa. Vile vile, amelaani matumizi ya nguvu kama njia ya kupambana na maandamano hayo

Bomba la gesi lashambuliwa Sinai ya KaskaziniPicha: AP

Kwa upande mwingine, nchini Misri washambuliaji wasiojulikana wameripua bomba la kusafirishia gesi linalopitia Sinai ya Kaskazini, eneo lililo karibu na Israel. Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya televisheni ya taifa nchini Misri. Redio ya Israel inasema, bomba hilo lililo karibu pia na Ukanda wa Gaza husafirisha gesi kwenda Jordan na kwamba gesi ya Israel haikuathirika.

Lakini ripoti za awali zilisema, bomba hilo husafirisha gesi ya Jordan na Israel vile vile. Wakaazi wa mji wa El Arish nchini Misri, wanasema kuwa moto mkubwa unawaka pembezoni mwa bomba hilo la gesi. Kwa mujibu wa duru za usalama, jeshi la Misri limeweza kuzima usambazaji wa gesi hiyo na sasa linapambana na moto.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW